Habari Kutokanyumba la Watawa Mukanisa la Orthodoksi Mtakatifu Nektario Mudji wa Kolwezi Inchi la Kongo Baada Zaire (Σουαχίλι, Swahili)
18 Αυγούστου 2009
KUTWAA KIPAWA LA KITAWA KWA BINTI
Katika inchi la Kongo na Mudji Kolwezi kuna Mama mtawa wa kwanza jina lake Thekla,anakaa kukanisa la Mtakatifu NEKTARIO, naye ni mtawa wa kwanza katika Afrika mzima tokeya mwaka 1988. Mpaka leo alikuwa na watawa ine,kwa mapendo ya Mwenyezi mtawa wa tano anaongezeka mu mwezi wa saba 2009 Hivi kipawa la kitawa kilitwala kwa Mwaskofu wa Katanga Mweshimiwa Meletio.
Mtawa wa sasa alipata jina la AGNIESE, ni mtoto wa padiri,ana na miaka 24, Alikuwa najifunza kunapita miaka tano karibu na wa tawa wengine kanisani.
Hizi habari za kupasha Neno la Ukweli katika Kiorthodoksi ni mambo Ya MIUJIZA katika myoyo yawa ndugu wenye AFRIKA CHINI LA SAHARA.
Ni furaha katika Bwana kwakuwona Ngufu la Roho Mtakatifu na kutumikisha wa tumishi wa Bwana hama Mwaskofu Katanga Mweshimiwa Meletio mtoka mlima takatifu la Athosi mu Monastari Grigoriou, yeye alimpiana marehemu padiri Kosma, Mpaka leo anaendelesha na kupasha NENO LA UKWELI, na kubatiza ma elfu ya wa pagani,na kujenga makanisa pamoja na ma nyumba la wa padiri ,tena anajenga ma masomo,kwanza primari,sekundari,masomo la kazi na lamikono,wanafunzi wanakuja ma elfu,walimu wengi,ivi tunamwomba Bwana asaidiye kazi lake liendeleye na watumishi wa haki wakudje shambani lake watumike.